Shughuli imemalizika katika dimba la Azam Complex, Chamazi wenyeji Azam Fc wakishindwa kutamba nyumbani dhidi ya Wauaji wa Kusini, Namungo Fc kufuatia sare ya 1-1.
Wanalambalamba wameshindwa kupata ushindi kwenye mchezo wa tatu mfululizo kwenye Ligi Kuu bara baada ya sare ya (0-0 vs Coastal Union), sare ya (2-2 vs Simba Sc) na sare ya (1-1 vs Namungo Fc)
FT: Azam FC 1-1 Namungo FC
⚽ 12’ Hamisi Nyenye
⚽ 43’ Sillah