Barabara Nne Kufungwa Dar Kupisha Mkutano wa SADC na EAC...




DAR: Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar, limetangaza kuzifunga kwa muda barabara nne zinazoingia katikati ya Jiji kutokana na Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wanaotarajiwa kukutana kesho, Jumamosi Februari 8,2025

Taarifa hiyo imeeleza barabara zitakazofungwa ni; Barabara ya Nyerere kutokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwenda katikati ya Jiji, Barabara ya Sokoine, Kivukoni na Lithuli kuanzia taa za Gerezani kwenda Hoteli ya Johari Rotana, Hyatt Regency hadi Ikulu, Barabara ya Ohio kutokea Kivukoni kwenda Hoteli ya Serena na Barabara ya Garden kutokea Barabara ya Lithuli kwenda Hoteli ya Southern Sun

Aidha, taarifa hiyo imesema kuwa zitafungwa kwa muda na kufunguliwa haraka na Bodaboda na bajaji zimezuiliwa kuingia kwenye maeneo katikati ya jiji hasa barabara zilizotajwa kwa muda kwa sababu za kiusalama wakati wa ugeni.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad