Bernad Morrison Ana Kamdomo Sana, Afunguka Haya Baada ya Kufungwa 6




“AKUTENDAYE mtende, mche asiyekutenda” hivi ndivyo tunaweza kusema hasa kwa alichokifanya mchezaji wa zamani wa Klabu ya Yanga ambaye kwa sasa ni mali ya Klabu ya Ken Gold Benard Morson, kutokana na kauli alizozitoa kabla na baada ya mechi ya Yanga dhidi ya Ken Gold iliyopigwa jana katika Uwanja wa KMC Complex jijini Dar es Salaam.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram siku chache kabla ya mechi, Morrison aliweka picha yake iliyoambatana na maelezo mafupi ya kuikejeli klabu ya Yanga, aliandika “Jumatano tutabadilisha tu jina letu kuwa ‘MC KENGOLD’ ili tupate matokeo mazuri dhidi ya utopolo. Kwasababu wanaogopa majina yanayoanza na MC”

Waswahili wanasema “ukiniletea dharau, nitaichukua nitaitunza kwa ajili ya matumizi ya baadaye” siku ikafika mechi ikapigwa na KenG old wakapigika goli 6 – 1 na kuifanya Yanga kupanda nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Morrison hakukata tamaa akarudi tena na kuandika “Kwa sababu tu ya hii post ndogo niliyofanya, nyie mlitaka kuwaua uwanjani jamani. Hamna shida we plan again”


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad