BREAKING: Aliyepinga Uteuzi wa Samia Kugombea Urais 2025 Afukuzwa CCM

BREAKING: Aliyepinga Uteuzi wa Samia Kugombea Urais 2025 Afukuzwa CCM


Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro kimetangaza kumfukuza Mchungaji Godfrey Malisa kutoka kwenye chama hicho kuanzia Februari 10, 2025, kwa tuhuma za kukika katiba na maadili ya chama.

Uamuzi huo umeelezwa kuwa umetokana na kauli zake za kupinga uamuzi wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa uliofanyika Januari 19, 2025. Malisa alidai kuwa uteuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan (Tanzania Bara) na Dkt. Hussein Mwinyi (Zanzibar) kuwa wagombea wa nafasi zao ulikiuka Katiba ya CCM.

Mchungaji Malisa, ambaye amewahi kugombea urais, uspika na ubunge, alijiunga na CCM mwaka 2021 na pia alikuwa mmoja wa makada tisa waliochukua fomu ya kugombea uenyekiti wa chama hicho mwaka 2022.

Katibu wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Merce Mollel, amesema kuwa uamuzi huo umefikiwa katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ya mkoa.

Hata hivyo kulingana na tovuti ya Mwananchi, Malisa amesema hakushirikishwa wala kupewa taarifa kuhusu kufukuzwa kwake, akisisitiza kuwa hana ufahamu wa uamuzi huo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad