Kiungo wa Simba Fabrice Ngoma amefikia makubaliano binafsi na klabu ya Al-Ittihad Tripoli ya Libya.
Jana Ngoma amepokea ofa nono ya Mshahara na Sign-on fee kutoka Al-Ittihad na tayari amesema ndio✅
Kilichobaki ni makubaliano kati ya Simba na Al-Ittihad,na muda wowote kuanzia sasa klabu hiyo tajiri ya Libya itatuma ofa Msimbazi.
Mkataba wa Ngoma na Simba umebakiza miezi mitano hivyo kisheria anaruhusiwa kuongea na timu yeyote.
Dirisha la usajili la Libya litafungwa mwishoni mwa mwezi huu na Al-Ittihad wanamuhitaji Ngoma ASAP!
Kama Simba watakubaliana na ofa ya Al-Ittihad basi nyota huyo ataondoka haraka sana.
Baada ya kukamilisha usajili wa Mahmoud Kahraba kutoka Al Ahly,saaa Ittihad wamemgeukia Ngoma.