Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi imefuta adhabu ya kadi nyekundu (Red Card) kwa mchezaji wa Namungo, Derick Mukombozi aliyoadhibiwa na mwamuzi wa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Namungo dhidi ya Simba.
Kamati imefikia maamuzi hayo baada ya kujiridhisha kuwa maelezo yaliyopo kwenye ripoti ya mwamuzi hayana ushahidi wa kutosha unaoendana na marejeo ya picha mjongeo kuwa Mukombozi alistahili kadi nyekundu.