Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imesema mchezo kati ya Simba SC dhidi ya Azam FC utafanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam Februari 24, 2025 saa 1:00 usiku.
Mchezo huo ulipangwa kufanyika kwenye Uwanja wa KMC Complex Februari 24, 2025 kuanzia saa 10:00 jioni.
Bodi ya Ligi imesema sababu ya mabadiliko hayo ni kutoa nafasi kwa mashabiki wengi zaidi kuhudhuria mchezo huo.