Diamond Platnumz, kupitia Instagram Stories, ameweka wazi kuhusu uvumi unaoendelea juu ya msanii wake Mbosso. Ameeleza kuwa wamefanya mazungumzo mazuri na kufikia maelewano kuhusu kusimamia rasmi kazi za Mbosso. Hata hivyo, ameomba mashabiki wawe na subira hadi tamko rasmi litakapotolewa.
Kwenye ujumbe wake, Diamond aliandika:
"Tumekuwa na Mazungumzo Mazuri na @mbosso_ namna ya kuanza rasmi sasa kusimamia kazi zake na tumekamilisha jambo letu vizuri sana. Tafadhali story yoyote inayozungumzwa kuhusu jambo hili la @mbosso_ naomba zipuuzwe, mpaka mimi binafsi na @mbosso_ tutakapotoa tamko rasmi."
Ujumbe huu umeongeza hamu kwa mashabiki ambao wanafuatilia mustakabali wa Mbosso ndani ya WCB Wasafi. Mashabiki wanasubiri kwa hamu tangazo rasmi kutoka kwa @diamondplatnumz na Mbosso ili kufahamu hatua inayofuata.