Dili Alilowekewa Mzize na Timu ya Al Ittihad ni Kufuru Tupu




Klabu ya Al Ittihad ya ligi kuu soka nchini Liby imetenga ada ya uhamisho ya zaidi ya TSh bilioni 3 kwaajili kumnasa mshambuliaji wa klabu ya Yanga Clement Mzize ambaye amewaka sana kwa siku za karibuni.

Al Ittihad mbali na fungu hilo la uhamisho wamemuwekea mezani Mzize ada binafsi ya kusaini mkataba (sign-on fee) ni zaidi ya TSh bilioni 1.3 na mshahara wa Tsh Milioni 50 kwa mwezi huku wakimshawishi kusaini mktaba wa miaka miwili kinda huyo wa zamani wa timu za vijana za Yanga.

Wakati hayo yakiendelea nje ya uwanja, Mzize ndiyo kwanza ananogesha biashara na kuwapa presha waarabu hao baada ya jana kufunga goli moja kati ya manne waliyoshinda dhidi ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad