Edo Kumwembe Amtetea Chasambi 'Ni Mchezaji Mzuri Kuliko Mutale'




“Naona Yanga wanafurahia kweli kweli jambo hili. Wanamchonganisha Chasambi na timu yake bila ya kujali sana masilahi ya taifa. Chasambi akikubali kutoka mchezoni basi tutakuwa tumempoteza mmoja kati ya vijana wazuri ambao siku za usoni wangeweza kutubeba kule Taifa Stars.

Ni kijana ambaye anahitaji mwendelezo wa ubora katika timu kama Simba ambayo ina mechi nyingi za Kimataifa kumkomaza. Baadae ataibuka tu kuwa tegemeo katika timu ya taifa kwa sababu ana kipaji kizuri miguuni.

Hata mechi timu yake yenyewe itakumbukwa kwa tukio lake la kujifunga lakini ukitazama kwa jumla wake, alikuwa na mechi bora na katika safu ya ushambuliaji wa Simba ni afadhali umpange yeye kuliko Joshua Mutale. 😅 Huu ndiyo ukweli.
.
Tusimtoe mchezoni. Mutabaribu hazina ya taifa. Kuna wachezaji hawawezi kuhimili kile kinachoandikwa dhidi yao.”

— Legend, Edo Kumwembe.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad