Web

Edo Kumwembe: Wachezaji Wetu Wazawa ni Wanyonge....



“Tanzania imechelewa sana hii. Labda staa wa Yanga na timu ya taifa ya Burkina Faso, Aziz Ki ndo ametuleta hapa majuzi. Amekwenda kumuoa mrembo maarufu nchini, Hamisa Mobetto.
.
Kwa nini imetokea kwa mara ya kwanza nchini? Shika peni uandike sababu. Kwanza kabisa wanasoka wa kigeni wanaokuja nchini sio wanyonge sana wa maisha. Wana kitu kinachoitwa ‘exposure’. Wanaishi maisha ya kujichanganya.
.
Hawaangalia sana wapi walipokulia na kutokea. Wanajaribu kuishi kama wanadamu wengine wenye nyadhifa mbalimbali. Mara nyingi nikitoka ‘out’ katika sehemu nzuri, huwa nakutana na wachezaji wa kigeni. Sikutani na wachezaji wazawa.
.
Huwa nakutana na Aziz Ki. Pacome Zouzoua, Clatous Chama, Ben Morrison. Serge Wawa , Moses Phiri na nyota wengine wa kigeni. Hauwezi kumkuta mchezaji wa kizawa katika maeneo haya labda awe ameitwa na kiongozi wa klabu yake anayekunywa hapo.
.
Wachezaji wetu wazawa ni WANYONGE. Hawataki kuyaacha maisha waliyokulia. Kwa sasa wana vipato vikubwa, lakini bado wanatawaliwa na hofu ya maisha. Kwao, Hamisa anaishi maisha tofauti na wao hata kama ametoka kuchukua pesa ya usajili Sh200 milioni.
.
Katika maisha haya ya kutoka katika sehemu nzuri, kukaa sehemu nzuri, kupiga picha sehemu nzuri, wanasoka wetu wameshindwa kujitengenezea hadhi maalumu ‘self branding. Wachezaji wetu wa kigeni hawana hofu na maisha haya.
.
Nachelea kusema labda sababu ni kipato. Kwamba wachezaji wa kigeni wanalipwa zaidi. HAPANA. sio kweli. Siku hizi wachezaji wetu wanalipwa pesa ndefu za mishahara, lakini ‘signing fee’ zao pia ni kubwa.
.
Upande wa wasanii wetu wao ni tofauti. Wanatoka maisha kama ya wachezaji wetu, lakini wanajua namna ya kujitengeneza kuwa mastaa wakubwa hata kama wana vipaji vya kawaida tu. Wana jua namna ya kujiongeza na kuwa wakubwa zaidi.”

— Legend Edo Kumwembe [via Mwnanachi]

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad