Web

Gambo: Kama Mtu Anataka Ubunge Asubiri Tuingie Uwanjani


Gambo: Kama Mtu Anataka Ubunge Asubiri Tuingie Uwanjani


Mbunge wa Arusha mjini Mrisho Gambo amejibu kilichotokea jana February 24,2025 kwenye baraza maalumu la jiji la Arusha la kupitisha bajeti baada ya madiwani kumtaka Mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Makonda kugombea ubunge jimbo la Arusha mjini muda utakapofika

Gambo kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari amesema kwamba kwa sasa yeye ndiye mbunge halali wa jimbo na kama kuna mtu ana tamani asubiri muda ufike waingie uwanjani aone kama ngoma ya kitoto kama ina kesha

“Tuna uzoefu na mambo ya kisiasa wala hatuna wasiwasi wowote na ukiona mtu anatafuta madiwani anawatengeneza wamuombe agombee madiwani wana nafasi yao wanaweza kumchagua mwenyekiti wa Halmashauri au wakamchagua Meya ila mbunge anachaguliwa na wajumbe pamoja wananchi,kama kuna yeyote yuko tayar tunamkaribisha tuko imara”-Gambo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad