Young Africans Sc imepanga kumsajili nyota wa kimataifa wa Gambia na Azam Fc Gibril Sillah [26] ifikapo dirisha kubwa la usajili,inaelezwa kuwa Young Africans imeanza kufanya mazungumzo na uongozi pamoja na menejimenti ya mchezaji kuona uwezekano wa kuinasa saini yake ifikapo dirisha kubwa la usajili.
.
Gibril Sillah atasajiliwa kuja kuziba pengo la Clement Mzize ambae anatarajiwa kuondoka Yanga Sc kuanzia sasa mpaka dirisha kubwa la usajili litakapofika.
.
Baadhi ya vilabu kama Wydad Athletic,Al Ittihad kutoka Libya zinaendelea kuwasiliana na mchezaji pamoja na uongozi wake ili kuona nani atafanikiwa kuinasa saini yake,inaelezwa Wydad Athletic imekua na ushawishi mkubwa kuliko Al ittihad kutokea Libya.
.