Web

Hakika Ikangalombo ni Mashine, Tunachomdai ni Magoli tu sasa



Body balance iko pale,kasi ya umeme iko pale,miguu yake inaweza kucheza kwenye maeneo finyu,ni mwepesi wa kuachia mali kwenye maeneo hatari,anatumia miguu yote hivyo anaweza kucheza winga zote mbili.

Ndani ya dakika 20 alizocheza ame pre-assist goli la Aziz lakini pia Aziz amemnyima assist ya wazi kama angeitumia vizuri ile low cross.

Ikangalombo ni “speed merchant” anapenda sana kukimbia pembeni kwenye “channel” hivyo akipata kiwanja kizuri kama Benjamini Mkapa,watu watalala na viatu.

Msiniambie nimemuona leo,mimi nilimuona huyu Jamaa kwenye fainal Za CHAN pale Algeria akiwa na Maxi na Mpanzu….hivyo najua nini naongea.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad