SOKA LETU LINAZIDI KUPIGA HATUA
Miaka 15 nyuma ilikuwa ni mara chache unasikia taarifa za wachezaji wazawa kuhitajika katika klabu za Afrika ya Kaskazini ama Kusini, wengi walikuwa wanaenda kwa mualiko kufanya majaribio.
Kwa sasa hadithi imekuwa tofauti, wachezaji wengi kutoka ligi ya Tanzania tena wazawa wanahitajika katika klabu za nje ya Tanzania kwa gharama kubwa, mfano wa klabu kama vile Wydad Casablanca,Kaizer Chiefs na nyinginezo.
Hii haikuja kwa bahati inatokana ukuaji wa soka letu eneo la (broadcasting) ligi kuonekana LIVE, eneo la wafadhili na wawekezaji katika klabu bila kusahau mamlaka za soka kama TFF na Bodi ya Ligi bila kusahau ushirikiano kutoka Serikalini.
Kwa sasa zipo taarifa za wachezaji Clement Mzize,Kibu Dennis, Feisal Salum kuhitaji katika klabu za nje ya Tanzania tena kwa fedha lukuki, hakika kazi kubwa inafanyika kwenye mpira. Ni majuzi tu kijana Selemani Mwalimu ameuzwa kwenda Wydad Casablanca.