Web

Hali ya Papa Francis Sio Nzuri, Vatican Yaanza Maandalizi ya Mazishi




Kiongozi wa Kanisa Katoliki, Papa Francis, mwenye umri wa miaka 88, anaendelea kupata matibabu kwenye Hospitali ya Gemelli jijini Rome baada ya kugunduliwa na nimonia kali. Ripoti zinadai kuwa walinzi wa Uswisi wanaolinda Vatican wameanza mazoezi ya maandalizi ya mazishi yake, jambo linalozua taharuki kwa waumini wa kabisa katoliki.

Kwa mujibu wa #Vatican, Papa Francis anasumbuliwa na maambukizi ya kupumua yanayojumuisha pumu, na madaktari wamemwekea mpango wa matibabu kwa kutumia antibiotiki. Pamoja na ugonjwa huu, hali yake inaangaliwa kwa umakini zaidi kutokana na historia yake ya kiafya, kwani aliwahi kuondolewa sehemu ya mapafu yake alipokuwa kijana.

Taarifa kutoka kwa watu wa karibu na Papa zinadai kuwa amewahi kusema, "Huenda safari hii nisimudu," jambo linaloashiria utayari wake wa kukabiliana na hatima yake. Hata hivyo, bado anapata lishe, anasoma magazeti, na anaendelea na kazi zake akiwa hospitalini.

Waumini wengi wameanza safari kuelekea hospitalini humo kumuombea kiongozi wao mkubwa wa kiroho, huku ulimwengu ukifuatilia kwa makini maendeleo ya afya yake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad