Hata Matajiri Wanakimbia Matunzo ya Watoto, Ona Elon Musk Akilalamikiwa na Mama Wake
Mama wa watoto watatu wa Elon Musk, mwimbaji Grimes amelalamika kwenye mtandao wa X kuwa Elon hapokei simu zake na mtoto wao anaumwa sana na anahitaji matibabu haraka,
Grimes ameandika, 'Ninasikitika kufanya hivi hadharani lakini sio sawa kuendelea kupuuza hali hii, Ikiwa hutaki kuzungumza nami unaweza tafadhali kuteua au kuajiri mtu anayeweza ili tuweze kusonga mbele katika kutatua hii dharura, Elon',
Watu waliouliza zaidi kuhusu tatizo la mtoto, Grimes alijibu, 'Sitatoa maelezo zaidi, hapokei simu, sms au emails zangu, nahitaji kuwasiliana nae sasa hivi, ili kumwokoa mtoto lasivyo atapata madhara ya muda mrefu, atakama inabidi nitumie guvu kwenye mitandao',