Nyota wa klabu ya Simba Sc Ladack Chasambi amewaomba radhi viongozi pamoja na wanachama vilevile mashabiki wa klabu hiyo kwa kujifunga goli na kusababisha timu kukosa alama tatu katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Fountain Gate.
Katika maelezo yake kupitia ukurasa wake wa mitandano ya kijamii, Chasambi amesema.
"Nawaomba radhi kwa uongozi wa klabu, benchi la ufundi, wachezaji wenzake na zaidi ya yote, mashabiki na wapenzi wa Simba kutokana na makosa aliyofanya kugharimu timu yetu"