Mshambuliaji wa klabu ya Wydad AC Seleman Mwalimu raia wa Tanzania anaenda kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza michuano ya kombe la Dunia la klabu katika muundo mpya.
Michuano hiyo inatarajiwa kufanyika nchini Marekani na Wydad AC ni miongoni mwa klabu ambazo zitashiriki michuano hiyo wakiwa kundi moja na Manchester City,Al Ain na Juventus.