Web

Kaa Kiaskari..Tanesco Watangazia Mikoa Hii Kukosa Umeme


Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetangaza mpango wa maboresho katika Kituo cha Kupokea, Kupoza, na Kusambaza Umeme cha Ubungo kilichopo jijini Dar es Salaam.

Kazi hizi zitafanyika kuanzia Jumamosi, Februari 22 hadi Ijumaa, Februari 28, 2025. Wakati wa utekelezaji wa maboresho haya, baadhi ya maeneo ya Zanzibar, Dar es Salaam, na Pwani yanatarajiwa kukosa umeme kwa nyakati tofauti.

Kulingana na ripoti ya Millard Ayo, Februari 19, 2025, TANESCO imeeleza kuwa hatua hii inalenga kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja kutokana na ongezeko la mahitaji ya umeme katika maeneo husika.


Kituo cha Ubungo kimezidiwa na mahitaji, hivyo shirika limeamua kufunga mashine mpya kubwa yenye uwezo wa MVA 300 ili kukidhi mahitaji hayo.

Aidha, katika kipindi hiki, TANESCO itafanya matengenezo mbalimbali ya miundombinu ya umeme ili kuhakikisha uimara wake hasa katika msimu wa mvua unaokuja.

Shirika linaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza wakati wa maboresho haya na linawahakikishia wateja kuwa taarifa za maendeleo zitatolewa hadi kukamilika kwa kazi hizi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad