Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), #JosephKabila, amemshutumu Rais wa Sasa #FélixTshisekedi kwa kusababisha mgogoro unaoendelea mashariki mwa nchi hiyo. Kwa mujibu wa Kabila, utawala wa Tshisekedi umekuwa ukiukwaji wa Katiba, kubana upinzani, na kuleta ukosefu wa utulivu wa kitaasisi, hali inayochochea machafuko zaidi.
Kabila pia ameonya kuwa mzozo wa M23 hauwezi kutatuliwa kwa nguvu za kijeshi pekee, bali unahitaji suluhisho la kina linalozingatia historia na matatizo ya msingi ya usalama nchini. Hata hivyo, amepinga madai ya serikali kwamba M23 ni kundi la vibaraka wa mataifa ya kigeni bila madai halali.
Mgogoro wa DRC unaendelea kuzua wasiwasi mkubwa wa kiusalama na kisiasa, huku mashirika ya kimataifa yakitaka mazungumzo ya amani kurejesha utulivu katika eneo hilo.