Kagame Ahofia Kupinduliwa, Mpango Wasukwa






Rais wa Rwanda Paul Kagame sasa anadai kuna njama ya kuishambulia nchi yake na kuipindua serikali anayoiongoza.

Amedai mpango huu unapangwa na majeshi ya DRC, chini ya amri za Rais wa nchi hiyo, Felix Tsishekedi, akisema Tsishekedi amelitangaza hili mara kadhaa.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo, hii ndiyo sababu ya vita visivyoisha vinavyoongozwa na majeshi ya DRC katika eneo la Goma, mpakani na Rwanda.

Rwanda inasema Tsishekedi pia anatumia vikosi vya SAMIDRC, wanajeshi wa Burundi, kundi la waasi la FDLR na mamluki wa Kizungu, kulifanikisha hili.



Rwanda imekanusha madai ya kuwafadhili waasi wa M23. [Picha: Hisani]

"Taarifa za hivi karibuni kutoka Goma zinaonyesha ushahidi wa maandalizi ya mashambulizi dhidi ya Rwanda, ambayo yamepangwa kwa kushirikiana na vikosi vya kigeni vinavyopigana mashariki mwa DRC, vikiwemo FDLR. Malengo yao hayakuwa tu kushinda M23, bali pia kuishambulia Rwanda," Rwanda imedai.

Taarifa hii imetolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya Rwanda, leo Jumapili.


Pia inadai kuwa SADC inahusika katika njama hii, na inalenga kuleta machafuko karibu na mpaka wa Kongo na Rwanda ili kuifanikisha njama hii.

Ameitaja hii kama sababu ya wanajeshi wake kutumwa mpakani, akisema lengo ni kuilinda nchi yake na raia na sio kuisaidia M23 inavyodaiwa.

Ikumbukwe kuwa Kongo imeilaumu Rwanda kwa kinachoendelea katika mji wa Goma, ambao umetekwa na waasi wa M23, ikidai wanafadhiliwa na Kigali.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad