Shughuli imemalizika katika dimba la Meja Jenerali Isamuyo Wenyeji huku JKT Tanzania wakifanikiwa kuwanyamazisha Wananchi wakigawana pointi kufuatia sare ya 0-0.
Wananchi wanasalia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu bara alama 46 baada ya mechi 18 walau kwa masaa 24 kusubiri Simba Sc wenyeji pointi 44 watafanya nini kwenye mchezo wake wa kesho dhidi ya Tanzania Prisons.
FT: JKT Tanzania 0-0 Yanga Sc
FT: KMC Fc 2-0 Singida Black Stars