Kocha wa zamani wa Yanga Sead Ramovic ambae kwa sasa anakinoa Kikosi cha CR Belouizdad ameanza kazi vibaya ndani ya Cr Belouizdad baada ya kupoteza mchezo wa Fainali ya Algeria Super Cup kwa kukubali kipigo cha penati 4-3 kutoka kwa Mc Alger kwenye uwanja wa Stade du 5 Juillet
Ramovic amekubali kipigo hicho baada ya sare ya 2-2 ndani ya dakika 90 akitoka nyuma kwa kusawazisha kipindi cha pili yaliyoifanya mechi hiyo kumalizika kwa sare ya 2-2
Magoli ya MC Alger yamefungwa na S. Bayazid 14' (P) na A. Abdellaoui 27 Kisha kipindi cha pili Belouizdad kusawazisha kupitia kwa A. Mahious 72' (P) na 88'.