Haji Manara amevunja ukimya wake baada ya mechi ya leo ya Yanga SC. Shughuli ilimalizika katika uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo huku JKT Tanzania walifanikiwa kuwanyamazisha wananchi huku waligawana pointi kufuatia sare ya 0-0. Wananchi wanasalia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu NBC Tanzania bara alama 46 baada ya mechi 18 walau kwa masaa 24 kusubiri Simba SC wenye pointi 44 watafanya nn kwenye mchezo wake wa kesho dhidi ya Prisons.
Baada ya Mechi hiyo, shabiki maarufu wa Yanga na Mkurugenzi wa Manara TV, Haji Manara amevunja ukimya wake kuhusu michuano hiyo. Kwa ameshukuru mungu kwa matokeo hayo na kudai kuwa bora aendelee na urubani wake kwenye mpira wa mtandao.
Ameomba msamaha Ladaki Chesambi kwa masimango, kejeli na dhihaka alizopokea kutoka kwa mashabiki wengi wa Yanga na hata Simba SC. Ameeleza kuwa sasa ni zamu ya Simba SC kuwadhihaki. Jambo ambalo limezua mijadala mbalimbali mitandaoni.