Jeshi la Polisi nchini Uganda linamshikilia Mtanzania Naima Omary kufuatia kifo cha Mchezaji soka wa Kimataifa wa Nigeria Abubakar Lawal (39) aliyekuwa anaichezea Vipers SC ya Uganda.
Naima anashikiliwa kwa uchunguzi kwakuwa alikuwa Mtu wa mwisho kukutana na Lawal February 24,2025 kabla ya kufariki kwa utata kutokana na kuwa na taarifa mbili tofauti kuhusiana na kifo chake, taarifa ya kwanza ilisema amepata ajali ya bodaboda lakini taarifa ya Polisi imeeleza kuwa amedondoka kutoka kwenye barcony ghorofani alipokuwa amekwenda Voice Mall maeneo ya Bwebajja, barabara ya kuelekea Entebbe kuonana na Naima.
Lawal inaelezwa alifika Voice Mall akiwa na gari yake yenye namba za usajili UBQ 695G na kwenda kukutana na Naima aliyekuwa anaishi hapo toka February 20, 2025 chumba namba 416 ambapo inaelezwa Naima alimuacha Lawal chumbani akiandaa chai.
Naima yupo nchini Uganda kwa ufadhili maalum (Scholarship) kwa ajili ya kuendeleza kipaji chake kucheza Basketball katika Chuo cha St Marry’s nchini Uganda.