Kivuli cha cleansheets kinaficha sana madhaifu ya Moussa Camara. Nimehesabu alama 7 za Simba zimepotea kwa sababu yake msimu huu. Kwenye mechi dhidi ya Yanga, alifanya makosa yakiyopelekea Simba kufungwa goli na Max Nzengeli; Simba akaacha alama 3.
Mechi dhidi ya Coastal Union, alifungwa goli na Hernest Malonga kwa positioning mbovu, liliopekea Simba kuacha alama mbili dhidi ya wagosi wa kaya. Na jana, goli la Zidane alikosea kufanya maamuzi na kusabisha Simba kuacha alama mbili nyingine.
Jumla hizo ni alama 7 Simba kapoteza kwa ajili yake. Huu mjadala wa cleansheets sio kigezo cha kuchukua tuzo ya golikipa bora Moussa Camara; kwa makosa aliyofanya, hastahili hii Tuzo. Ana makosa mengi sana yanayosabibisha magoli.