Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mheshimiwa Said Mtanda amejitoa kwenye maandalizi ya Pamba kuelekea mchezo wa Ligi kuu kandanda Tanzania bara dhidi ya Yanga.
Mlezi huyo ambae ni shabiki wa yanga Kindaki ndaki amewaachia jukumu hilo viongozi wengine wa Pamba ambao ni mashabiki wa Simba ili wahakikishe ushindi unapatikana na ahadi ya ushindi au sare kwa Pamba iko pale pale.