Web

Kocha Moalin Nyuma ya Pazia Mafanikio ya Yanga....

Kocha Moalin Nyuma ya Pazia Mafanikio ya Yanga....



Yanga ni wajanja sana na kwa kijiweni kuna kauli yetu unatakiwa uwe umesoma Cuba ili uweze kuwashtukia walivyo na hesabu ndefu na mipango ya kiandamizi. Wakati wanamchukua Abdihamid Moalin walituzuga jamaa anaenda kuwa mkurugenzi wa ufundi lakini kumbe walishatumia akili ya Cuba katika uamuzi wa kumchukua kocha huyo kutoka KMC.

Kwanza ana leseni daraja A ya Caf inayomruhusu kuwa kocha mkuu wa timu inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara hivyo kama ingetokea kocha mkuu anaondoka, ingekuwa ni rahisi kwa Moallin kuongoza jahazi. Ndivyo ilivyotokea pale Kocha Sead Ramovic alipoamua kuachia ngazi ghafla na kwenda Algeria na Moalin alibeba jukumu la kuiongoza timu hiyo katika mechi ya ligi dhidi KenGold Februari 5 ambayo Yanga ilishinda mabao 6-1.

Kingine ambacho Yanga inafanikiwa kwa Moalin ni uzoefu mkubwa alionao wa soka la Tanzania ambao ameupata katika timu za Azam na KMC ambazo amezifundisha kabla ya kutua Jangwani. Uzoefu huo umemfanya aifahamu vyema Yanga na kikosi chake kwa vile alilazimika kukifuatilia na kukifanyia tathmini mara nyingi kipindi alipokutana nacho kwenye mechi za Ligi hivyo hana ugeni nacho kwa sasa.

Pia anazifahamu timu nyingi za Ligi Kuu kwani tayari amekutana nazo kabla hajajiunga na Yanga na anajua vyema mazingira ya soka la Tanzania hivyo anakuwa msaada kwa kocha mkuu ambaye ni mgeni.

Huu muendelezo wa vipigo na kufanya vizuri ambao Yanga wamekuwa nao siku za hivi karibuni sidhani kama ni jambo linalotokea kwa kubahatisha au juhudi za kocha mkuu peke yake ambaye ni mgeni. Naona kuna mkono wa bwana Abdihamid Moalin ambaye sasa hivi sio mtu wa kusimama sana mbele ya kamera za waandishi wa habari.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad