"Kuna wachezaji wamenipigia simu wamekerwa na hali iliyotokea juzi maana wachezaji wana malengo ya kushindana na hawafurahishwi na kikosi ambacho kilipangwa juzi kuwa sio cha ushindani."- Patrick Aussems.
"Wakati nipo Singida kabla ya mechi na Yanga ile wiki mambo mengi ya ajabu yalitokea kila jioni nilikuwa nampigia simu Boss na nilijua kabla kuna uhusiano kati ya Singida na Yanga na baada ya pale nilijua kuwa siwezi kukaa Singida Black Stars maana mimi ni mtu mshindani napenda kushindana."- Patrick Aussems.
"Unawezaje kuwa na malengo ya kushindana halafu hutaki kushindana na timu kama Yanga?, Hi haiwezekani na wakati nilipoondoka Singida BS tulikuwa nafasi ya pili na niilijua tu lazima timu itashuka."- Patrick Aussems.
Kocha Patrick Aussems amezungumza kwenye CROWN SPORTS ya @crownfmtz