Web

Kocha wa Simba Fadlu Davids Aitamani Yanga....



Kocha wa Simba Fadlu Davids amesema mechi mbili zijazo zinaweza kutoa picha halisi ya ubingwa kwa timu yake msimu huu.

Fadlu amesema kama watapoteza mechi hizo basi timu yake itakuwa imejiweka kwenye hatari kubwa ya kupoteza ubingwa, kwani itakuwa imepoteza pointi nyingi na itakuwa ngumu kumfikia aliyeko kileleni.

“Mechi kubwa zilizopo mbele yetu ni hizi za sasa dhidi ya Yanga na Coastal, hizi zingine tumeshamalizana nazo, lakini napata wakati mgumu kutokana na rekodi za mzunguko wa kwanza.

“Kwa sasa akili zipo katika mbio za ubingwa kwani bado ziko wazi na mwanga unaonekana ila tukifanya makosa mechi mbili zijazo nuru itazima kabisa.

“Hizi kwetu ni mechi zinazobeba ajenda ya ubingwa na hatutacheka nazo kabisa, kwani tunahitaji alama sita za nguvu zitakazotuweka katika nafasi nzuri.” -Amesema Fadlu davids

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad