Web

Kocha Yanga; Mashabiki wa Yanga ni Wakipekee Africa Sijawahi ona




"Hatujaja hapa kwa likizo. Tunaiheshimu Pamba lakini tuko hapa kushinda. Hakuna kingine zaidi ya kushinda na kupata alama tatu. Tunajua mchezo hautakuwa rahisi, lakini tuko tayari kupambana. Timu zote zinapocheza dhidi yetu zinatoa kila kitu. Kesho tunatarajia mchezo mgumu, lakini sisi ni Yanga, na tunapaswa kuonesha kuwa sisi ni timu kubwa.

Ningependa kusema kitu kuhusu mashabiki wa Yanga. Nina uzoefu mkubwa wa soka barani Afrika, nimefanya kazi na vilabu vikubwa, lakini mashabiki wa Yanga ni wa kipekee. Siogopi kusema hivi kwa sababu ni ukweli. Wananipa mshangao mkubwa na furaha kubwa. Wanapokuja kwa wingi kutuunga mkono, wanatupa motisha kubwa zaidi ya kupambana, kufanya kazi kwa bidii mazoezini, na kutoa kila kitu uwanjani.

Nina neno moja kwao: Bravo, bravo, bravo!

Kocha Mkuu Miloud Hamdi

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad