Web

Kuhusu Kuwa X wa Hamisa Mobetto, Ally Kamwe Kaanika Kila Kitu Hadharani

 

Kuhusu Kuwa X wa Hamisa Mobetto, Ally Kamwe Kaanika Kila Kitu Hadharani

NDOA ya mastaa wawili, wa soka Stephane Aziz KI na mfanyabiashara na mjasiriamali, Hamisa Mobetto bado imebaki vichwani mwa watu, wengi wakiendelea kuwapongeza kutokana na kufanikisha jambo hilo muhimu katika maisha yao.

Ndoa hiyo pia imeacha mjadala kutokana na ustaa wa wawili hao na wamewahi kuhusishwa kimapenzi na mastaa wengine ikiwamo Hamisa na Ali Kamwe.

Hata hivyo, pamoja na kuzungumzwa mengi juu ya uhusiano huo, lakini kwa taarifa tu, Ali Kamwe hajawahi kutoka kimapenzi na mwanadada huyo na zaidi ni kirafiki.

Ofisa huyo wa habari wa klabu ya Yanga amewapongeza wawili hao kwa kumsifu kiungo mshambuliaji wao, amepata mke, lakini akifichua kwa upande wake mambo ya ndoa, watu watasubiri sana kwani hana mpango kwa miaka ya karibuni.

Ali Kamwe amekiri mahusiano ya kimapenzi ni changamoto kwake na hawezi kuyamudu kwa sasa, ndiyo maana bado hajaingia huko.

Amesema ndoto yake ni kufunga ndoa baada ya kufikisha umri wa zaidi ya miaka 55, huku akiwashauri vijana kujenga maisha yao kwanza kabla ya kufikiria ndoa, akisisitiza wanawake wana vigezo vingi wanapochagua wenza wa maisha.

Pia, amewakumbusha kutoendeshwa na presha za kijamii, ikiwemo masuala ya umri, katika kufanya maamuzi ya ndoa.

KUHUSU HAMISA

Ameweka wazi hajawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamitindo Hamisa kama wengi walivyokuwa wakifikiria bali wao ni marafiki tu na kumpongeza mrembo huyo na kumtakia kila la heri katika ndoa yake, akimtaja kuwa mwanamke mwenye sifa bora za mke mwema.

“Mimi na Hamisa hatujawahi kuwa wapenzi. Tena kuna wakati ananifanyiaga mpango kabisa na huwa tunajadili kama kuna mwanamke mzuri niliyemuona na yeye ananichana kabisa kama anafaa au lah.

“Ujue suala la mahusiano naliheshimu sana, ndiyo maana sitaki kabisa kukurupuka, yanaweza kuniua najijua, hivyo bora nichelewe ili nikifa na miaka 57 huko wajue tu ni presha kutokana na umri mkubwa.

“Hili nataka kuliweka wazi kwa vijana wenzangu, mimi nilishawahi kuoa, hivyo naelewa, kwa hiyo ni bora ujijenge kwanza kabla hujaumizwa huko, wanawake wana vigezo vigumu sana, unaweza kuwa naye lakini usifae na usiwepo kwenye mipango yake.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad