Web

Kuipangia Singida Kikosi ni Kuinyuma Uhuru Timu....




Na mwandishi Lameck Sabaganga

Kwa mijadala ambayo nimeitazama inaendelea baada ya mchezo wa Yanga na Singida Black Stars inaonyesha kuwa asilimia kubwa ya watu walikuwa na matokeo ya Singida kushinda kwenye mechi hiyo.

Kikawaida mwalimu anaweza kupanga kikosi kulingana na mahitaji ya mchezo husika na namna ambavyo amewasoma wapinzani na sio mchezaji bora anaweza kuanza kwenye mechi.

Kinachoendelea kwasasa ni kuzinyima uhuru hizi timu za madaraja ya chini kuamua wachezaji zitakazowatumia kwenye michezo yake dhidi ya Simba na Yanga.

Hii pia ni aina moja wapo ya kudumaza soka letu. Yanga kwenye ubora wao kila timu imepata ilichokitegemea, kila timu imevuna ilichokipanda.Ili timu isiwe imepanga matokeo lazima iifunge Yanga? Na ikifungwa tu basi imepanga matokeo?

Tuwape uhuru makocha wa kuamua nyota watakaocheza kwenye michezo husika kulingana na mbinu za wapinzani wao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad