Kumbe Chama Ndio Sababu ya Kocha Romavic Kuondoka Yanga



Licha ya kupeleka ombi la kuvunja mkataba ili aondoke klabuni kwa kilichoelezwa amepata ofa nono kutoka CR Belouizdad ya Algeria, lakini kuna mambo kadhaa nyuma ya pazia katika dili la kocha Sead Ramovic kusepa Yanga ikiwa ni siku 82 tangu alipojiunga nayo Novemba 15, mwaka jana.

Ramovic aliyejiunga na Yanga kutoka TS Galaxy ya Afrika Kusini anakuwa kocha wa pili kuondoka Jangwani baada ya Miguel Gamondi aliyesitishiwa mkataba ndani ya msimu huu na kuridhiwa na Mjerumani huyo ambaye naye amesepa ndani ya muda mfupi.

Taarifa zinadai kuwa kulikuwa na mipango ya chini chini waliyokuwa nayo mabosi wa Yanga dhidi ya kocha huyo baada ya timu hiyo kushindwa kuvuka kwenda robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Hata hivyo, ofa iliyoelezwa ndio imemng’oa Ramovic ghafla kutoka Yanga ni kama kocha huyo amewawahi maosi wake, kwani kuna mambo matano yaliyokuwa yamng’oe kama ilivyokuwa mtangulizi wake, Gamondi.

Hapa chini ni mambo yanayodaiwa yalikuwa yale kichwa cha Ramovic kabla ya dili hilo kutoka CR Belouizdad inayoelezwa itamfanya awe analipwa mshahara mnono wa Dola 40,000 (zaidi ya Sh 101 milioni) tofauti na ule aliokuwa akiupokea Yanga, mbali na yeye kuilipa Yanga fedha za kuvunja mkataba.

MISIMAMO MIKALI

Tukio la kwanza ambalo lilianza kumtibulia Ramovic lilijiri pale Algeria ambapo wakati timu yake inajiandaa na kikao cha mwisho kuelekea mechi dhidi ya MC Alger alimuondoa Clatous Chama kwenye kikosi kinachoanza.

Chama aliondolewa baada ya kuchelewa kwenye lifti kwa dakika zisizozidi mbili, basi jamaa akamuondoa kwenye kikosi kinachoanza wakati tayari alishapanga na kikosi kizima kilishajua kwamba kiungo huyo anaanza.

Hatua hiyo iliwakera wachezaji wakiamini Chama alistahili kuanza mechi na si wachezaji tu, bali hata viongozi na baadaye Yanga ikapoteza kwa mabao 2-0.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad