Web

Kuna Namna Tuliaminishwa DUBE ni Straiker Mbaya, We Alimkwambia Nani?

Kuna Namna Tuliaminishwa DUBE ni Straiker Mbaya, We Alimkwambia Nani?


Em tumjadili kwanza Pacome kwanza Kwadikika kadhaa kabla ya kuendelea na mjadala wa Dube huyu Pacome kuna namna kama kuna siku anaamua tu leo wacha nicheze mpira wangu then kuna siku anawaangalia wengine namna wanavyo cheza leo sasa kaamua kucheza ule mpira wake tunaoujua.

Kuna ile Pasi alipiga katikati ya uwanja Mwili wake ukiwa umeangalia kwenye goli lake alipo Diara then Pasi akaipiga kwa Nyuma yake ilienda kwa Duke Abuya Nadhani what a Pass

DUBE:

Kuna namna kuna uongo tulazimishwa kuukubali kua Dube ni Striker Mbaya ambae Yanga inahitaji mtu mwengine zaidi yake ambae yupo bora zaidi yeye hatoshi kwasababu anakosa sana magoli.

Dube bila ya Penati hata Moja ameisaidia Yanga kupata Magoli 17 kupitia yeye mpaka sasa yaani akiwa na magoli 10 na kusaidia mengine 7 hakuna mchezaji aliyefanya hivi mpaka sasa kwenye ligi kuu Tanzania Bara hapo sizungumzii kwenye klabu Bingwa na FA anamagoli pia na assist.

Duniani hivi sasa ukitaja Mastriker bora wenye msaada wa magoli 15+ hawafiki 20 sasa achana na huko hapa kwetu mastriker wenye magoli 10 bila Penati ni Dube pekee yupo kwenye kiwango bora sana kuna namna tunalazimisha ajenda zetu kwenye Miguu yake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad