Web

Madawini Arusha Waomba Paul Makonda Agombee Ubunge

Madawini Arusha Waomba Paul Makonda Agombee Ubunge


Madiwani wa Baraza la Halmashauri katika Jiji la Arusha wamemuomba Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda agombee ubunge katika Jimbo la Arusha Mjini kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika October mwaka huu 2025.

Madiwani hao akiwemo Naibu Meya wa Jiji la Arusha Abraham Mollel na Diwani wa Kara ya Themi Lobora Petro wakiongea kwenye kikao maalumu cha Madiwani cha kujadili bajeti wamesema kuwa kwa namna Makondq anavyogusa Watu muda ukifika anatakiwa achukue fomu.

“Tunakaa na Watu wanasema kwa namna unavyogusa Watu, sisi tunakaa na Wananchi na wanazungumza mengi dhidi yako ikikupendeza vuta fomu, tuko nyuma yako chukua haya maneno endelea kutafakari wewe ni muombaji” —-Abraham Mollel, Naibu Meya Jiji la Arusha

Hata hivyo Mkuu huyo wa Mkoa Paul Makonda hakujibu chochote baada ya hoja hizo za Madiwani lakini awali wakati anaongea na Madiwani hao katika kikao hicho cha bajeti alitoa maagizo kwa Mkuu wa Wilaya kufuatilia tuhuma za baadhi ya Watumishi wanaodaiwa kufanya upigaji wa fedha Tsh. million 200.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad