ARUSHA: Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (#TAKUKURU) imeagizwa kumhoji aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Mrisho Gambo katika uchunguzi wao kuhusu upotevu wa Tsh. Milioni 400 zilizochangwa na Wadau kusaidia Bodaboda kwa kuwa alikuwa muasisi wa ukusanyaji fedha hizo
Maagizo hayo yametolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda Februari 27, 2025 wakati wa Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) alipohoji kuhusu fedha hizo na kueleza alipata malalamiko tangu akiwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi alipofanya ziara #Arusha
Ikumbukwe kwa nyakati tofauti, Gambo ambaye sasa ni Mbunge wa Arusha Mjini ameitupia lawama TAKUKURU kwa kutopata majibu ya walioiba fedha hizo huku akidai taarifa za benki zipo na zinaonesha waliozitoa, tarehe na hadi kiasi kilichotolewa, akiwatuhumu waliokuwa Viongozi wa Umoja wa Madereva Bodaboda Arusha (UBOJA)