Mama Aziz K Arusha Bomu Jingine, Avujisha Meseji za Aziz K Akimlalamikia Eng. Hersi




Mama yake Aziz Ki, katika muendelezo wa kutaka kutuonyesha kuwa Rais wa Klabu ya Yanga, Eng. Hersi Said si kiongozi mzuri na namna anavyo watreat wachezaji, amevujisha chati za Aziz Ki za WhatsApp ambazo aliwahi kumtumia Hersi kuhusu mkataba wake katika upande wa maboresho ukizingatia na ofa anazoendelea kupata kutoka kwenye vilabu vingine.

Kwa ufupi, Aziz anadai hakuwahi kufikiria kama kuna wakati utafika atakuja kuwa na tatizo na Hersi ama klabu kwasababu alipokuja kusaini Yanga, alikuwa na ofa nzuri zaidi ya klabu hiyo lakini alimfuata Hersi si tu kama kiongozi wa klabu lakini kama Baba tangu amchukulie kama sehemu ya familia yake.

Na alipokuja Yanga, Hersi alimuahidi Aziz Ki kumpa miaka miwili tu na hatomzuia kwenda kwenye vilabu vingine, miaka miwili ilimalizika na bado kukawa na ofa nzuri kutoka vilabu vingine, na aliamua kusalia Yanga na ukizingatia aliahidiwa ahadi nyingi kama angerenew mkataba lakini hakuna kilichowahi kutokea.

Aziz anadai alisaini mkataba ambao kimsingi ulikuwa na ofa ndogo ukilinganisha na ofa kutoka vilabu vingine, Ki alisaini bila kinyongo lakini baadae Hersi akaanza kumuona kama sio mchezaji yule ambaye alimsaini mwanzo.

Ki anadai hana furaha Yanga na alijitoa kwa juhudi zake zote akiamini watafika mbali kwenye klabu bingwa ila bahati mbaya haijawa hivyo, na porojo zote hizo Hersi akamtaka Ki aendelee kusalia Yanga, Ki anauliza, kwanini unanifanyia hivi Boss???

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad