Web

Mechi ya Kibabe Sana Yanga Vs Singida Black Stars Leo


Yanga vs Singida Black Stars


Unaweza kusema hii ni mechi ya kibingwa. Yanga yenye pointi 49 baada ya mechi 19, inapambana kuongeza pengo zaidi dhidi ya Simba yenye 47 ikishika nafasi ya pili ikicheza michezo 18.
.
Singida BS iliyotoka kuvunja rekodi ya JKT iliyokuwa timu pekee ambayo haikupoteza nyumbani msimu huu kabla ya kula la 1-0 lililowekwa kimiani na mshambuliaji mpya wa timu hiyo, Jonathan Sovah aliyeanza Ligi Kuu na moto mkali, nayo inahitaji pointi tatu zitakazowaweka sehemu nzuri zaidi katika msimamo kwani inafahamu ikipoteza kuhatarisha kukaa nafasi ya nne kwa kasi ya Tabora Utd.
.
Ikumbukwe mchezo huu utamkutanisha Kocha Miloud Hamdi na Singida aliyokuwa akikinoa tangu Disemba 30, 2024 kabla ya kutambulishwa Yanga Februari 4, 2025 akichukua mikoba ya Sead Ratnovic.
.
Kipindi chote ambacho ligi ilisimama kuanzia Disemba 28, 2024 kabla ya kuendelea Februari Mosi 2025, Kocha Hamdi alikuwa kambini Arusha akisuka mipango na kikosi cha Singida, hivyo ni wazi anawafahamu vizuri sana wachezaji wa timu hiyo kuliko wa Yanga aliokaa nao kwa takribani siku 12.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad