Web

Msimamo wa Ligi Kuu Baada ya Yanga Kushinda 5-0 Dhidi ya Mashujaa



Msimamo wa Ligi Kuu NBC Tanzania bara umeweza kubadilika kiasi baada ya mechi ya leo. Singida BS waliweza kuenda sare ya 2-2 dhidi ya Pamba Jiji FC. Mashujaa FC walipokea kichapo kikali cha 5-0. Aidha Namungo FC walienda sare ya 0-0.

Young Africans wapo kwenye nafasi ya kwanza kwenye Msimamo wa Ligi Kuu NBC Tanzania bara kufuatia ushindi wa mabao 5-0 leo. Wapo na pointi 55. Simba SC wapo kwenye nafasi ya pili. Azam FC wapo kwenye nafasi ya tatu.

Young Africans leo pia wamepata ushindi mkubwa dhidi ya Mashujaa FC. Mechi hiyo ilikamilika kwa mabao 5-0. Inadaiwa kwamba Yanga wanatambua Ligi ya msimu huu ni ngumu, hivyo wanaandaa kila silaha ili kushinda hii vita kubwa ya 2024/2025. Ligi ya msimu huu haijulikani itaamuliwa kwa pointi au magoli hivyo Yanga wanaset kila kitu kiwe katika upande wao.

Hadi sasa Young Africans wamecheza mechi 21 za Ligi na wamefanikiwa kufunga magoli 55 goli 14 zaidi ya Simba SC.

Katika mechi ya leo, Jumapili Februari 23 dhidi Mashujaa FC, Clatous Chama amefunga magoli mawili wakati wananchi, Yanga SC wakiishindilia Mashujaa FC Jumla ya magoli 5-0 katika uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.

Wananchi wameendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu NBC Tanzania bara kufuatia ushindi wa leo. Wana pointi 55 baada ya mechi 21 huku wazee wa mapigo na mwendo wakiendelea kusalia nafasi ya 9 alama 23 baada ya mechi 21. Abuya alifunga bao lake dakika ya 32, Dube 48, Aucho 54 na Clatous Chama alifunga mabao mawili katika dakika ya 74 na 83.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad