Abal Khasim 🗣."Ni kweli ligi yetu ina viungo wengi bora wa ndani na kutoka mataifa mbalimbali lakini kwangu Mudathir ni bora licha ya kutokuwa mtulivu lakini upambanaji wake umekuwa ukimpa nafasi ya kuonekana mchezaji bora na muhimu,” anasema na kuongeza:
“Mudathir ni mpambanaji sio mchezaji wa kukubali kushindwa amekuwa imara na ndio maana kila kocha ambaye amepita ndani ya kikosi cha Yanga tangu ameungana nayo amekuwa akipata nafasi ya kucheza.”