Ndege ya Marekani Yapinduka Canada Matairi Juu




Watu 15 akiwemo Mtoto, wamejeruhiwa huku baadhi yao wakiwaishwa Hospitali kutokana na majeraha waliyoyapata baada ya Ndege ya Delta ya Nchini Marekani kupata ajali leo kwa kubinuka juu chini kwenye njia ya kurukia Ndege baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Toronto Nchini Canada.

Hata hivyo hakuna kifo chochote kilichosababishwa na ajali hiyo ambayo imehusisha Ndege ya Delta namba 4819 iliyotokea Minneapolis Marekani kwenda Toronto, Canada ikiwa na Abiria 80 ambao wote wameondolewa kwenye Ndege hiyo tayari.

Kubinuka kwa Ndege hii kumetokea wakati upepo mkali ukiripotiwa katika Jiji la Toronto kwa siku nzima ya leo.

Ni ajali ambayo imetokea katika kipindi cha chini ya wiki tatu toka Ndege nyingine kupata ajali kwa kugongana angani na helikopta ya Jeshi la Marekani ilipokuwa ikikaribia kutua katika uwanja wa ndege uliopo Washington DC na kuua Watu wote waliokuwemo ndani yake.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad