Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa Amjibu Donald Trump, "South Afria Haikuhusu"




Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amemjibu Rais wa Marekani Donald Trump aliyetangaza kusitisha misaada nchini humo kisa madai ya ukiukwaji wa haki za Binadamu na Wazungu kunyanyaswa na kupokonywa ardhi wanazomiliki ambapo Ramaphosa amemtaka Trump aache kuingilia mambo ya Afrika Kusini kwakuwa hayamuhusu na kusema ardhi ya Afrika Kusini sio ya Trump hivyo hana haki ya kuwapangia cha kufanya.

Ramaphosa amesema “Hii ishu ambayo Donald Trump anaiogopa sana, hii ardhi ni ya kwetu, sijui Donald Trump anahusika vipi na atafanya nini kuhusu ardhi ya Afrika Kusini kwasababu hajawahi kuwa hapa, aitunze America yake na tutaitunza Afrika Kusini yetu, Afrika Kusini ni ardhi yetu na inamilikiwa na Watu wote wanaoishi Afrika Kusini, Afrika Kusini haimilikiwi na Donald Trump”

“Nikikutana na Trump nitamwambia, nitamwambia wewe Trump ni Mtu mbaya kwasababu unapendelea upande mmoja, Marekani kulikuwa na Watu wenye asili ya Marekani waliwaondoa na kuwaua karibu wote, sisi tunaishi kama Taifa la wote Watu weusi na weupe na tunatafuta suluhisho sisi wenyewe kuhusu ardhi, Trump atuache, atuache”

“Wakati tukiwa tunakandamizwa na kunyanyaswa (na Makaburu ) hakuwepo hapa, hakupigana bega kwa bega na sisi na sisi wenyewe tulitatua tatizo kwa msaada wa Watu wengine Duniani Trump hakuwepo, kwahiyo aendelee na mambo yake White House na tutaendelea na mambo yetu, pambana na mambo yako na sisi hatutoingilia mambo ya Marekani”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad