Rais wa Shirikisho la Soka nchini 🇨🇲Cameroon Samuel Eto'o ameshinda kesi yake dhidi ya Shirikisho la Soka Barani Africa [CAF], iliyomzuia kuwania nafasi ya ujumbe kwenye kamati ya Utendaji ya Shirikisho hilo.
Hata hivyo Rais huyo wa Fecafoot alitozwa faini ya USD 200,000 [TZS 514 MILLION] kwa kosa la kuvunja na kukiuka kanuni za Shirikisho la soka Barani Afrika.
Uchaguzi wa Rais na wajumbe wa kamati ya utendaji wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) unatarajiwa kufanyika mnamo mwezi March,2025.