Web

Simba Imepania Kumsajili Maxi Nzengeli Kutoka Yanga

Simba Imepania Kumsajili Maxi Nzengeli Kutoka Yanga



Nyota wa kimataifa wa Congo na Yanga Sc Maxi Mpia Nzengeli inasadikika atatua Msimbazi kwa mujibu wa taarifa iliotufikia,Maxi Nzengeli anamalizia mkataba wake wa mkopo maalumu ndani ya Klabu ya Yanga hivyo mwishoni mwa msimu huu haki zote zinarejea kwa Klabu yake ya Maniema ya Congo kuamua hatima ya mchezaji.
-
Simba wamefungua mazungumzo rasmi na Maniema juu ya kuinasa huduma ya Maxi Nzengeli kuja kuitumikia Simba katika dirisha kubwa la usajili.
-
Kila kitu kwasasa kipo katika hatua za awali huku Maxi mwenyewe akiwa ni sehemu muhimu juu ya makubaliano yoyote iwe Simba au Yanga, Chanzo chetu kinasema kipaumbele chake ni dakika za kucheza zaidi, Maxi anataka kucheza muda mwingi uwanjani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad