Klabu ya Singida Black Stars imeeleza kustushwa na taarifa za Kocha wao Mkuu, Hamdi Miloud Raia wa Algeria na Ufaransa kutambulishwa kama Kocha mpya wa Yanga bila kufuata utaratibu.
Singida Black Stars walimtangaza Hamdi Miloud kuwa Kocha wao mpya mwezi mmoja uliopita kwa Mkataba wa mwaka mmoja na nusu huku Yanga Sc jana Februari 04, 2025 wakimtangaza kocha huyo kuwa kocha wao mkuu mpya akichukua mikoba ya Sead Ramovic ambaye ameondoka kwa makubaliano ya pande zote mbili.