Sinto Shangaa dirisha lijalo nikamuona akiwaniwa na timu kubwa kama ataendelea na mwendelezo bora kwenye ligi katika michezo iliyosalia
Seleman Salim Rashid 'Bwenzi' kwenye mechi tatu mfululizo za ligi kuu Tanzania tangu atue Kengold, amefunga mabao matatu ndani ya dakika 189.
Vs Tabora
Vs Yanga
Vs Fountain Gate
Sio kwa bahati mbaya anauwezo mzuri mguuni, nguvu,ufundi wa kuchezea mpira, uhakika wa kulenga lango na kufunga lakini pia ubora wa kupiga mipira iliyokufa (Faulo,kona,free-kick)
Rejea magoli yake akiwa Champions
Vs Biashara akiwa Mbeya kwanza,
Vs FGA akiwa na Tma n.k
Huyu amewahi kucheza ligi kuu akiwa na Namungo mrejeeni vizuri mtanielewa.
Kwenye ligi kwa sasa analingana nao Mishamo Daudi Michael na Herbert Charles Lukindo ambapo Mishamo amecheza mechi 16, dakika 1323 na Lukindo mechi 15, dakika 943.
Selema Salim Rashid amejiunga na Kengold Januari 2025 akitokea Mbeya Kwanza ya championship.