Afisa habari wa Yanga Ali Kamwe amekanusha uvumi wa taarifa za kuwa mchezaji wao mpya Ikangalombo anaidai Yanga na ndio maana hachezi.Kamwe amesema kuwa taarifa hizo sio za kweli.Ukweli ni kuwa Ikangalombo anatafuta utimamu wa mwili na akiwa sawa ataanza kucheza.
”Hilo swala kuwa Ikangakombo anadai sio kweli hatudai chochote.Ikangalombo fitness(utimamu wa mwili) wake upo chini. Hata kocha aliyepita Ramovic alisema. Kocha wetu Hamdi kesho akiona anamuhitaji kwenye mechi yetu dhidi ya KMC FC mtamuona na asipohitajika basi hamtamuona.”
- Ali Kamwe, Afisa habari Yanga.