Meneja wa habari na mawasiliano klabu ya Simba SC Ahmed Ally amevunja ukimya wake kuhusu goli la kujifunga la Ladaki Chesambi. Kulingana na taarifa tulizozipata hivi sasa, mechi hiyo dhidi ya Fountain Gate ilikamilika kwa sare ya 1-1. Ahmed Ally amepatia Ladaki Chesambi ushauri kuwa leo amekuwa mtu mzima wa kimpira. Ameeleza kuwa ingekua kimaumbile basi leo ndio siku ya kubaleghe.
Amemshauri Ladaki Chesambi kuwa licha ya dhihaka, kejeli na matusi huo ni ukaribisho kwenye ukubwa wake. Ameeleza kuwa ameumiza mioyo ya Wanasimba lakini ameeleza kuwa yeye sio wa Kwanza.
Mwisho Meneja wa habari na mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally ameshauri mashabiki, uongozi na wachezaji wa Simba kukasirika lakini wasimchukie mchezaji huyo maarufu.
Aidha kocha mkuu wa klabu ya Simba SC, Davids Fadlu amesema kuwa leo haikuwa siku njema kwa Simba SC. Pia amezungumzia goli la kujifunga la Ladaki Chesambi na kudai kuwa hastahili kulaumiwa bali kusaidiwa ili ajifunze zaidi.